BAADA ya kuandamwa na skendo kuwa anatoka kimapenzi na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, mkali wa Bongo Fleva, Meninah Ab...

BAADA ya kuandamwa na skendo kuwa anatoka kimapenzi
na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, mkali wa Bongo Fleva, Meninah
Abdulkareem ‘Meninah la Divah’ amesema yuko mbioni kumtambulisha mchumba
wake.
Meninah Abdulkareem ‘Meninah la Divah’.
Akipiga stori, Meninah ambaye ni zao kutoka shindano
la kuibua vipaji vya kuimba, Bongo Star Search ‘BSS’ 2012 alisema;
“Nimechoshwa kila siku kusikia Diamond,
sasa ni bora nimtafute mwanaume yeyote tu kisha nimtambulishe ili
ijulikane siko na Diamond,” alisema Meninah ambaye yupo mbioni kuachia
ngoma mpya ya Kaniganda.
Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa Meninah anatoka kimapenzi na
Diamond, pia Diamond ameshafika kwao kujaribu kutoa mahari ili amuoe.