Archive Pages Design$type=blogging

MBARONI KWA KUCHEZA WAKIWA UCHI KWA STAILI YA KIGODORO

WATU wanne wakazi wa eneo la Masasi Mbovu (Masasi ya zamani) mjini Masasi wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kucheza uchi, kwa...

WATU wanne wakazi wa eneo la Masasi Mbovu (Masasi ya zamani) mjini Masasi wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kucheza uchi, kwa staili inayoitwa Kigodoro kwenye sherehe ya ndoa.

Mkuu wa Polisi wilayani Masasi, Ndagile Makubi jana alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa juzi jioni katika eneo la Masasi mbovu watuhumiwa kutokana na kucheza wakiwa watupu kunakokiuka maadili ya Kitanzania.

Alisema walipata taarifa za kuwepo kwa tukio hilo la kiudhalilishaji kutoka kwa wasamaria wema waliokuwepo kwenye sherehe hizo na kwamba Polisi walifika na kufanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa hao waliokutwa wakiwa wanaendelea kutoa burudani hiyo kwa mamia ya watu waliojitokeza kwenye sherehe hizo wakiwamo watoto.

Makubi aliwataja wanaoshikiliwa na jeshi hilo kuwa ni pamoja na Anna Yohana (25), Jemima Jordan (22), Aziza Chukachuka (20) na mtoto wa miaka 17 (jina linahifadhiwa) wote wakiwa ni wakazi wa mjini Masasi mkoani Mtwara.

Alisema uchunguzi unaendelea na kwamba watakapobainika kuhusika na tukio hilo la udhalilishaji hasa kwa jinsia ya kike watafikishwa mahakamani kwa taratibu zingine za kisheria.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Tiba Matwani na Fatuma Hamisi wamepongeza Polisi wilayani Masasi kwa kuanza operesheni hiyo na kwamba vitendo hivyo vinavyofanywa na wanawake wenzao havistahili kuachiwa vikiendelea kwa kuwa vinadhalilisha utu wao.

Aidha, Kamanda Makubi alizungumzia mikakati iliyowekwa na jeshi hilo mjini humo, ikiwa ni pamoja na kuendesha operesheni maalumu kwenye maeneo yote ya burudani na sherehe mbalimbali ili kuwabaini watu wote wanaokwenda kinyume na maadili ya Kitanzania.

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: MBARONI KWA KUCHEZA WAKIWA UCHI KWA STAILI YA KIGODORO
MBARONI KWA KUCHEZA WAKIWA UCHI KWA STAILI YA KIGODORO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhsRWZzcFE1cDSASL5ONPfNRFwniH6JXLdwGJ__NbxnbvtSIh_v9ZD8RPCHCxzIhyXUiYOEb6_jQlLs9NDLDoAz_tcL9fw1sCK_1InIbvLVz7lhNRFvtvJHzudV7TxLlS4rmhmbPIPgv0i-/s1600/moko.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhsRWZzcFE1cDSASL5ONPfNRFwniH6JXLdwGJ__NbxnbvtSIh_v9ZD8RPCHCxzIhyXUiYOEb6_jQlLs9NDLDoAz_tcL9fw1sCK_1InIbvLVz7lhNRFvtvJHzudV7TxLlS4rmhmbPIPgv0i-/s72-c/moko.jpg
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/10/mbaroni-kwa-kucheza-wakiwa-uchi-kwa.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/10/mbaroni-kwa-kucheza-wakiwa-uchi-kwa.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago