MSANII mkongwe katika gemu la filamu Bongo, Lucy Komba amefunguka kwamba baada ya kufunga ndoa hivi karibuni ameishi na mumewe Janus ...
MSANII
mkongwe katika gemu la filamu Bongo, Lucy Komba amefunguka kwamba baada
ya kufunga ndoa hivi karibuni ameishi na mumewe Janus kwa wiki mbili
tu.
Akizungumza na paparazi wetu, Lucy alisema kwa sasa amebaki Bongo
peke yake ikiwa ni baada ya mumewe kwenda kwao Denmark ambapo alitakiwa
kurudi kazini lakini bado anafanya maandalizi ili amfuate.
“Mume wangu alikaa kwa wiki mbili tu baada ya kufunga ndoa
nikamwambia aniache ili nimalizie kufanya maandalizi ya kumfuata huko
kwao Denmark ambapo mpaka sasa sijajua nitaenda lini maana bado
sijamaliza mambo yangu ila tunaaminiana na tumeshazoea kwani tangu
wakati wa uchumba tulikuwa tuko mbalimbali lakini nitaenda.
“Nikienda huko nitakaa kwa miezi mitatu nitarudi hapa Bongo kusalimia
na kukaa kama wiki kadhaa, nampenda sana mume wangu na ninammis kwa
kweli,” alisema Lucy Komba.