HABARI mpya kutoka kwa mastaa wanaodaiwa kuvunjika kwa ndoa yao, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ na Gardner G. Habash ‘Kaptaini’, in...
HABARI
mpya kutoka kwa mastaa wanaodaiwa kuvunjika kwa ndoa yao, Judith
Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ na Gardner G. Habash ‘Kaptaini’, inasemekana
wamevunja mkataba wa kuendesha Mgahawa wa Nyumbani Lounge uliopo Ada
Estate, Kinondoni jijini Dar.
Mbongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’.
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, wawili hao walidaiwa kufikia uamuzi
wa kuvunja mkataba baada ya kuona ndoa yao inasuasua kutokana na
migogoro.“Lady Jaydee au Jide alipoona mambo yanakwenda ndivyosivyo
alimshauri Gardner wavunje mkataba wa Nyumbani Lounge ili kila mmoja awe
na businesses (biashara) zake.
“Walimfuata mmiliki wa jengo, wakamwambia kwamba wanavunja, akawakubalia,” kilinyetisha chanzo makini. Chanzo hicho kilizidi kwenda mbali zaidi na kudai kuwa mgahawa huo kwa sasa unamilikiwa na mzungu.
‘Lady Jaydee’ na Gardner G. Habash ‘Kaptaini’ wakati wakiwa pamoja.
“Mgahawa kwa sasa unamilikiwa na Mzungu mmoja ambaye amenunua baadhi
ya vitendea kazi walivyokuwa wakivitumia na Jaydee amekuwa akimsaidia
mzungu huyo baadhi ya mambo kwa kuwa ni mgeni Bongo ila sasa Nyumbani
Lounge itafunguliwa kwa jina jipya la M.O.G na Jaydee atafanya shoo ya
ufunguzi kama msanii tu,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kushibishwa maelezo hayo, mwanahabari wetu alimtafuta Jide bila mafanikio lakini Gardner alipopatikana, alijibu kwa kifupi.
“Siwezi kuzungumza chochote katika suala hilo.”
Jide na Gardner wanadaiwa kutengana na kila mmoja akiishi kivyake lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha.