post-feature-image
HomeBurudani

KUNA MADHARA YA KUISHI PAMOJA KABLA YA KUOANA?-2

Ni wiki nyingine tunapokutana tena katika ukurasa wetu huu mzuri, kubadilishana mawazo kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo uhusian...


Ni wiki nyingine tunapokutana tena katika ukurasa wetu huu mzuri, kubadilishana mawazo kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo uhusiano wa kimapenzi. Mada tuliyokuwa tumeianza wiki iliyopita ilikuwa ikihoji kwamba je, kuna madhara ya kuishi pamoja kabla ya kuoana?
Maoni yamekuwa mengi, kila mmoja anasema lake. Wapo ambao wamekubaliana na mimi kwamba si vizuri kuishi pamoja kabla hamjaoana ingawa wapo wengine ambao wamesema ni sawa kuishi pamoja kabla ya kuoana kwa sababu wao wanaishi hivyo kwa kipindi kirefu.
Mimi si mjuaji wa kila kitu ndiyo maana nikataka tubadilishane mawazo, kila mtu aseme vile anavyojua na mwisho, tuhitimishe kwa pamoja. Nilianza kukueleza kwamba sababu ya kwanza inayofanya kitendo cha kuishi pamoja kabla ya kuoana kisiwe sawa, ni vigumu zaidi kwa watu wanaoishi pamoja kuoana ingawa wapo ambao waliishi pamoja namwisho wakaoana.
Sababu ya pili nilikueleza kwamba kama wewe ni mwanamke, mwanaume wako hataiona thamani yako kwa kuwa umekubali kuishi naye kienyeji bila kufuata utaratibu na sababu ya tatu tuliyoijadili, ni kwamba mume wa kweli hapendi mteremko.
Wanaume wengi ambao wanatafuta wake wa kuishi nao, hawapendi wanawake ambao wanajirahisi au ambao wanawapata bila jasho. Sasa ikiwa wewe mwanamke kabla hata mpenzi wako hajakuchumbia tayari umeshahamishia nguo zako kwake, atajisifia nini mbele za wenzake?
Ataamini wewe ni mwanamke mwepesi ambaye mwanaume yeyote anaweza kukupata kwa urahisi. Muache mumeo mtarajiwa ahangaike kukupata ikiwa ni pamoja na kuja kwa wazazi wako au ndugu zako. 
4. ATAKUOA KWA SABABU YA SHINIKIZO
Ni ukweli usiofichika kwamba watu wanaoishi pamoja, shinikizo kutoka kwa watu wanaowazunguka kuhusu kuoana huwa kubwa sana. Kila siku ndiyo utakuwa wimbo, ‘utanioa lini?’, mwisho ili kukwepa usumbufu, mwanaume huamua kuoa ili tu kumridhisha mwanamke na siyo kwa sababu anampenda. Matokeo yake ni kuingia katika ndoa ambayo haikuwa na ridhaa kutoka pande zote mbili.
5. NI RAHISI KUPEANA TALAKA
Mkianza kuishi kabla ya kuoana, maana yake ni kwamba mtazoeana sana mapema, kila mmoja atayajua mapungufu ya mwenzake na ni hapo ndiyo kukoseana adabu kutakapoanza na mwisho mtaishia kupeana talaka.
NINI CHA KUFANYA?
Ukiwauliza watu wengi wanaoishi pamoja bila ndoa, majibu yao watakwambia bado wanajipanga kwa maana ya kutafuta mahari, kujenga nyumba au kutafuta fedha za harusi. Hata hivyo, kikwazo kikubwa kwa wengi kimeonekana ni suala la mahari na gharama za ndoa.
Kama wewe na mwenzi wako mnapendana kwa dhati, mambo haya hayatakiwi kuwazuia kuoana. Mnaweza kuamua kupanga kufunga ndoa yenye sherehe ndogo ambayo haitawagharimu fedha nyingi. Hata suala la mahari, mnaweza pia kuzungumza na wazazi wa pande zote mbili ikawa inalipwa kwa awamu.
Hakuna suala linaloleta heshima kwenye jamii kama kufunga ndoa halali. Si hivyo tu, hata mbele za Mungu, watu wanaosihi bila ndoa maana yake wanazini na kuvunja amri ambazo zimewekwa na Mungu. Kwa nini uishi kwenye dhambi? Chukua hatua sasa, andaeni mipango mfunge ndoa.
Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: KUNA MADHARA YA KUISHI PAMOJA KABLA YA KUOANA?-2
KUNA MADHARA YA KUISHI PAMOJA KABLA YA KUOANA?-2
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi0hujhWjB-XDmJXzdGWVgyz9NxJYaQwhG9sdz5wtksToh6_ywXy_KInMaS6eTkrCI89nHu9XYc2AsP90mgvA5X6HVOtwO6VZ_m77yMGe0poTNtmGexS9r1QrIDkULq0Dl6JygvxtqjUbA/s1600/aa9eed643fc044c49d9f6f6c51d2a0f4.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi0hujhWjB-XDmJXzdGWVgyz9NxJYaQwhG9sdz5wtksToh6_ywXy_KInMaS6eTkrCI89nHu9XYc2AsP90mgvA5X6HVOtwO6VZ_m77yMGe0poTNtmGexS9r1QrIDkULq0Dl6JygvxtqjUbA/s72-c/aa9eed643fc044c49d9f6f6c51d2a0f4.jpg
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/10/kuna-madhara-ya-kuishi-pamoja-kabla-ya.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/10/kuna-madhara-ya-kuishi-pamoja-kabla-ya.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago