Stori: Gladness Mallya Haijakaa poa! Katika kuonesha kwamba anakwenda na fasheni za...
Stori: Gladness Mallya Haijakaa poa!
Katika kuonesha kwamba anakwenda na fasheni za mambele, staa wa sinema
za Kibongo, Husna Idd ‘Sajent’ amezua balaa baada ya kutinga kivazi
kilichomuacha wazi sehemu kubwa ya maungo yake.
Staa wa sinema za Kibongo, Husna Idd ‘Sajent’.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri hivi karibuni
katika sherehe moja kwenye Ukumbi wa Dar West uliopo Tabata, Dar ambapo
Sajent alikuwa ametinga gauni ambalo liliacha wazi sehemu ya matiti na
mapaja.
Kufuatia kigauni hicho, baadhi ya watu walibaki wakimshangaa na
kumzungumzia huku wakijiuliza kwa nini alitinga kigauni hicho lakini
mwenyewe aliendelea na yake.