Hit maker wa ‘Dear God’, Kala Jeremiah amepinga vikali kuwa amepotea kwenye game toka alivyohit na wimbo...
Hit maker wa ‘Dear God’, Kala Jeremiah amepinga vikali kuwa
amepotea kwenye game toka alivyohit na wimbo wa ‘Dear God’, huku akidai
kuwa huu ndio mwaka ambao ameingiza pesa nyingi kuliko miaka mingine
aliyokaa kwenye muziki.
Akizungumza leo, Kala amesema licha ya kutoonekana akifanya
show kwa wingi mwaka huu, lakini ameingia mikataba mingi na makampuni
mbalimbali.
“Mwaka huu ni mwaka mzuri kwangu kuna mikataba nimeingia, si kweli
sijapotea, ni mitazamo ya watu, ukweli ni kwamba mwaka huu kwangu
umekuwa mwaka wa baraka, wa neema mwaka wa mavuno kwahiyo ni mwaka mzuri
kwangu ninaweza kusema. Kibiashara nimefanya vizuri mwaka huu,
inawezaka mwaka huu nikawa sijafanya show nyingi lakini kifedha nadhani
au kwa kipato mwaka huu ninaweza kusema nimeingiza kipato kikubwa kuliko
miaka yote niliyokuwa kwenye muziki,” alisema Kala.
Katika hatua nyingine Kala amewataka mashabiki wa muziki wake kusubiri muziki mzuri kabla mwaka huu haujaisha.
“Mashabiki wasubiri muziki mzuri tu, siwezi kusema ni ngoma gani inakuja wao wasubiri wataona,”