Muigizaji wa filamu Blandina Chagula aka Johari amesema pamoja na kusikitishwa kutokana na bodi ya...
Muigizaji wa filamu Blandina Chagula aka Johari amesema pamoja
na kusikitishwa kutokana na bodi ya filamu nchini kuizua filamu ya
‘Sister Marry’ isitoke, amekula hasara kubwa.
Johari amesema kuwa maandalizi ya filamu hiyo yalighalimu shilingi milioni 30.
“Unajua inauma sana, tumeshindwa kutetea filamu ya ‘Sister Marry’
kutokana na madai eti tumedhalilisha dini. Ina maana hawataki
tuzungumzie maisha halisi kwenye filamu zetu? Mimi binafsi imeniumiza
sana. Ile filamu imegharimu zaidi ya milioni 30, hebu angalia, Halafu
inafungiwa ili isitoke kabisa! Kinachonisikitisha ni kwamba serikali
yetu inashindwa kuangalia sisi tunavumbua baadhi ya maovu ya watu ambayo
wanayafanya ili kuelimisha jamii. Kwahiyo imefungiwa na kukatazwa
isitoke kabisa kwa sababu kuna mambo ya ukweli ambayo tumeyaonyesha.
Tumefanya kila njia mpaka sasa hivi tumeshindwa, kwahiyo filamu ya
Sister Marry haitatoka tena,” amesema Johari.