Kajala Masanja amekanusha uvumi ulioandikwa kwenye magazeti ya udaku kuwa amefungua kesi dhidi ya mama ya...
Kajala Masanja amekanusha uvumi ulioandikwa kwenye magazeti ya
udaku kuwa amefungua kesi dhidi ya mama yake mzazi na Wema Sepetu
kutokana kile kilichodaiwa kutukanwa na mama huyo kwenye sherehe ya siku
ya kuzaliwa ya Wema mwishoni mwa mwezi uliopita.
Kajala ambaye amesema yupo busy na kazi zake binafsi, amesema hana ugomvi wowote na Wema kama watu wanavyozusha. “Hapana
sijamfungulia mashtaka yoyote Mama Wema. Siwezi kufanya kitu kama hicho
mama ni mzazi, mzazi kama mzazi huwezi ukasema umrudishie kitu,”
amesema. “Mzazi anaweza akakutukana akakufanyia nini lakini still
atabakia kuwa mzazi. Sina ugomvi wowote na Wema, hayo mambo sasa hivi
hayapo ni kazi tu.”
Wema na mama yake