MSANII wa filamu Bongo, Wastara Juma amemuumbua msanii mwenzake Deogratius Shija baada ya kutoa taarifa zinazoonekana ni za uongo. Msa...
MSANII wa filamu Bongo, Wastara Juma amemuumbua msanii mwenzake Deogratius Shija baada ya kutoa taarifa zinazoonekana ni za uongo.
Msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma
Awali Wastara ambaye hivi karibuni alinyakua tuzo ya Muigizaji Bora
wa Kike wa mwaka kwenye tuzo za Action and Cuts, alimshukuru Mzee Majuto
kwamba ndiye aliyemtoa kisanaa jambo ambalo limemhuzunisha Shija na
kusema anashangaa kwa kuwa yeye ndiye aliyemtoa.
Kufuatia maelezo hayo, Wastara amesema, taarifa aliyoitoa Shija ni ya uongo kwani filamu ya kwanza kabisa alicheza na Mzee Majuto ndiyo maana alimshukuru, ya pili alicheza na Frank Mwikongi na ya tatu ndiyo ya Shija.
Msanii wa filamu Bongo Deogratius Shija
“Nimemshukuru Mzee Majuto kwa kuwa ndiye wa kwanza kunitoa, huyo
Shija nimecheza naye filamu ya tatu, sasa anacholaumu nini? Mimi huwa
sipendi lawama za kijinga,” alisema Wastara.