Msanii wa Sanaa ya Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiong...
Msanii
wa Sanaa ya Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Alipokuwa
akiitambulisha filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU ambayo
amewashirikisha Flora Mtegoha au Mama Kanumba na Msanii wa Muziki wa
Kizazi Kipya Linah Sanga.

Msanii
Wa Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiitambulisha
filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU leo mbele ya wanahabari
(hawapo pichani).,Kulia ni Mmoja kati wa wasanii walioshiriki katika
filamu hiyo ajulikanae kama Flora Mtegoha almaarufu kama Mama Kanumba

Meneja
Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Ltd, Evance Stephen akiongea na
wanahabari leo katika Ofisi za Proin Promotions Ltd zilizopo Mikocheni
mtaa wa Ursino wakati wa Utambulisho wa Filamu mpya ya Lulu Iitwayo
MAPENZI YA MUNGU.
Msanii Elizabeth Michael aka Lulu leo
ametambulisha Filamu yake Mpya ambayo imeingia sokoni leo iitwayo
MAPENZI YA MUNGU, huku akiwa amemshirikisha Msanii wa Bongo Fleva Linah
Sanga na Mama Kanumba.
Wakati akiilezea filamu hiyo leo mbele ya
wanahabari Lulu amesema Kuwa Ni Filamu inayofundisha na Kutoa somo kwa
mtu yoyote yule ambae yupo hapa duniani kwa kuendelea kuonyesha kuwa
MUNGU YUPO. Akiongezea kuwa..."Sisi kama binadamu tumekuwa tukifanya
mambo mengi sana hapa Duniani na kupelekea kumsahau Mungu na pengine
kuendelea kufikiria kuwa yote tuyafanyayo ni kwa uwezo wetu kumbe Sio
uwezo wetu na Ni Mapenzi ya Mungu tu ndio yanayofanya sisi kufikia hapa
tulipo leo"
Filamu ya MAPENZI YA MUNGU imekuwa gumzo
kabla ya kutoka kutokana na watanzania wengi kuwa na shauku ya Kutaka
kumuona Lulu tena mara baada ya Kuonekana katika Filamu Zake Mbili
zilizotangulia za FOOLISH AGE na FAMILY CURSE. Sasa Lulu kuonekana tena
katika kiwango cha Juu katika Filamu hii Mpya ambayo imeingia Sokoni
Leo.
Filamu ya MAPENZI YA MUNGU ni filamu inayosambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd.
Filamu ya MAPENZI YA MUNGU ni filamu inayosambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd.