Msanii mrembo wa Bongo Fleva, Meninah amezungumzia kwa mara ya kwanza tetesi za kuwa na uhusiano na Diamo...
Msanii mrembo wa Bongo Fleva, Meninah amezungumzia kwa mara ya kwanza tetesi za kuwa na uhusiano na Diamond Platnumz.
Meninah ameeleza ukweli wake kuhusu tetesi hizo.
“Unajua nimekuwa niangalia tu hayo mambo yanavyoenda hasa kwenye
magazeti lakini sielewi wao hizo habari wanatoa wapi maana naona
wanatengeneza hizo story mara sijui nimevishwa pete! Sijavishwa pete na
mtu yeyote yule wala sijawahi kuchat na mtu nikamwambia habari hizo.
Naona wanatengeneza sana suala hilo, mie sijui na mahusiano na Diamond,”
amesema.
“Kuniathiri kwangu halijaniathiri kwakuwa familia yangu inaelewa
ukweli kwamba hamna kitu kama hicho. Kumbuka mie bado naishi nyumbani
kwetu na nyumbani wananiamini na wala huyo Diamond hajawahi kunifutalia
wala kunitamkia. Yaani huwa namuona tu kwa mbali kwenye matamasha. Na
ngoma zangu nilikuwa natamani sana kufanya naye lakini nilikuwa
nashindwa hata kumfuta kumwambia sasa hivi mambo hayo yanavyozidi
kuendelea ndo kabisa. Halafu unajua Diamond ni msanii mkubwa sana
kwahiyo ukitaka kufanya naye kazi lazima ujipange halafu ukizingatia mie
bado sio msanii mkubwa kivile ila tokea zamani nilikuwa natamani sana
kufanya naye kazi ila kumpata kwake ndo nilishindwa,” ameongeza.
“Ila kiukweli huwa inaniuma sana kuzushiwa vitu ambavyo havina ukweli
wowote naona watu wa magazeti ndo wanalazimisha iwe ivyo kwakuwa
wanaona kila msichana mrembo lazima awe na Diamond. Sio sawa kuandika
vitu ambavyo sio vya kweli halafu hawana vithibitisho maana siku ya siku
hata mtu alikuwa hana mpango na wewe lakini ataona ‘mbona wananiandika
sana kuhusu huyu Meninah’ yule mwanaume unajua ndo watamfanya sasa aanze
kunifuatilia, maana Diamond ana mpenzi wake kila mtu anamfahamu Wema.
Na kuhusu sijui Wema kunitumia watu hamna kitu kama hicho, sijawahi
kutumiwa mtu yeyote yule kwahiyo napenda watu waelewe hivyo.”
Kwa upande mwingine muimbaji huyo amesema anatarajia kuachia wimbo mpya uitwao ‘Kaniganda’.