NDOA basi! Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amezima ndoto za kuishi maisha ya mke na mume kwa kudai ku...
NDOA basi!
Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’
amezima ndoto za kuishi maisha ya mke na mume kwa kudai kuwa, amebaini
kujiingiza kwenye ulimwengu huo ni kujipa ‘stress’ za kujitakia.
Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda juzi, Dida alisema baada ya kuachana
na aliyekuwa mume wake, Edzen Jumanne, amebaini wanaume wote lao ni moja
hivyo kama atakubali kuingia kwenye ndoa na mwanaume mwingine, itakuwa
ni yaleyale.
“Yani sasa hivi hata aje mwanaume na gia gani siwezi kukubali kuolewa tena, kwa kifupi sina ndoto za kuitwa mke wa mtu tena, bora nibaki peke yangu nifanye mambo yangu,” alisema Dida.
“Yani sasa hivi hata aje mwanaume na gia gani siwezi kukubali kuolewa tena, kwa kifupi sina ndoto za kuitwa mke wa mtu tena, bora nibaki peke yangu nifanye mambo yangu,” alisema Dida.