WASANII wawili waliowahi kuwa marafiki wa kupika na kupakua, Flora Mvungi na Salma Jabu ‘Nisha’ bifu lao sasa limefika pabaya baada ...
WASANII
wawili waliowahi kuwa marafiki wa kupika na kupakua, Flora Mvungi na
Salma Jabu ‘Nisha’ bifu lao sasa limefika pabaya baada ya hivi karibuni
kuwaacha watu midomo wazi kwa kitendo chao cha kupitana kama
hawafahamiani.
Msanii wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’.
Ishu hiyo ilitokea wikiendi iliyopita kwenye sherehe ya kumbukumbu ya
siku ya kuzaliwa ya staa wa filamu, Wastara Juma iliyofanyika katika
ukumbi wa Dar West uliopo Tabata jijini Dar es Salaam. Wawili hao
walikutana mlangoni wakati wa kuingia, lakini Flora alimpita Nisha kama
hamfahamu na kama hiyo haitoshi, walipoingia ndani, kila mmoja alikaa
meza yake.
Wakati sherehe zikiendelea, ukafika wakati wa kufungua shampeni na
baada ya tukio hilo, Nisha alipewa jukumu la kuwagawia wageni waalikwa
kwa kuwamiminia kwenye grasi zao, lakini alipofika kwenye meza aliyokaa
mwenzake, Flora alikataa glasi yake kuwekwa kinywaji hicho.
Msanii wa filamu Bongo, Flora Mvungi.
Baada ya tukio hilo, paparazi wetu aliwafuata mastaa hao na kuwauliza
kulikoni, na Flora alisema: “Sikumuona Nisha mimi, na shampeni
nimekataa kwa sababu huwa siipendi.”
Kwa upande wake, Nisha alisema: “Mimi sikumuona Flora, kuhusu Shampeni mbona nilimimina kwenye glasi zote jamani!”