KAZI sana! Mkazi wa Buguruni, Rukia Nassor amekimbilia Kituo cha Polisi Buguruni jijini Dar kutoa taarifa ya bintiye Saida Said (18) ...
KAZI sana!
Mkazi wa Buguruni, Rukia Nassor amekimbilia Kituo cha Polisi Buguruni
jijini Dar kutoa taarifa ya bintiye Saida Said (18) (pichani)kutoroshwa
nyumbani kwake siku chache kabla ya ndoa.
Alipofika kituoni hapo, mwanamke huyo alimtaja mtu mmoja kwa jina moja la Shaban kwamba ndiye aliyefanya kitendo hicho.
Alipofika kituoni hapo, mwanamke huyo alimtaja mtu mmoja kwa jina moja la Shaban kwamba ndiye aliyefanya kitendo hicho.
Bi harusi mtarajiwa, Saida Said (18) aliyetoroshwa siku chache kabla ya ndoa.
Akizungumza na Uwazi juzi, mmoja wa ndugu ambaye hakupenda jina lake
lichapishwe gazetini alisema mama huyo amekuwa akihaha kwa binti yake
kotoroshwa na mwanaume huyo tangu Septemba 25, mwaka huu ambapo kila
akimpigia simu hapatikana hewani.
Jeshi la polisi bado liko ndani ya msako
mkali ili kuhakikisha binti huyo anapatikana na hatua za kisheria
zinachukuliwa kwa mwanaume huyo.
Ndugu huyo alisema Saida alitarajiwa kufanyiwa ‘kitchen part’ Oktoba 31, mwaka huu na kufuatia na ndoa Novemba 6 huku ikidaiwa kuwa, upande wa bwana harusi michango inaendelea kama kawaida.
Jalada la uchunguzi kuhusu kutoroshwa kwa bi harusi huyo linasomeka Kumbukumbu; BUR/RB/10170/2014 KUTOROSHA.