Staa wa Bongo Movies, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’. SOMO! Staa wa Bongo Movies, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ ameibuka na k...
Staa wa Bongo Movies, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.
SOMO! Staa wa Bongo Movies, Lulu Semagongo ‘Aunty
Lulu’ ameibuka na kumtaka msanii mwenzake, Blandina Chagula ‘Johari’
kukubaliana na matokeo ya aliyekuwa mpenzi wake Vincent Kigos ‘Ray’
kwamba kwa sasa ana uhusiano na mtu mwingine.
Akistorisha na paparazi wetu, Aunty Lulu alimtaka Johari kukubaliana
na matokeo na aige mfano wake kwani aliachana na Bond Bin Sinan ambaye
kwa sasa ana mpenzi mwingine hivyo asimchukie Chuchu Hans anayetoka na
Ray kwa sasa kwani kuachana ni jambo la kawaida katika mapenzi hivyo
hatakiwi kuwa na kinyongo.
Msanii Bongo Movies, Blandina Chagula ‘Johari’.
“Mimi nimepitia kwenye maisha hayo ndiyo maana namshauri Johari
akubaliane na matokeo kwamba Ray kwa sasa yupo na Chuchu Hans na asiwe
na kinyongo naye ampende na aongee naye vizuri tu kwani ndiyo maisha,”
alisema Aunty Lulu.