SHEIKH Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa ameweka wazi kuwa msanii nyota wa filamu, Aunt Ezekiel ambaye aliolewa na S...

SHEIKH
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa ameweka wazi kuwa msanii
nyota wa filamu, Aunt Ezekiel ambaye aliolewa na Sunday Demonte hana
ndoa kutokana na kukaa mbali na mumewe kwa zaidi ya miezi sita.
“Hakuna ndoa kati ya mtu yeyote ambaye amezidi miezi 6 bila kukutana na mumewe kwa mujibu wa dini ya kiislamu.
Msanii nyota wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel
“Kwa kawaida mwanamke ambaye hajakutana na mumewe kwa miezi 6 au
zaidi baada ya ndoa yao, hupaswa kwenda mara moja Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (Bakwata) kulalamika na hatimaye kudai talaka, ikiwa mwanamke
ameridhika na hali hiyo, naye akaamua kukaa kimya huku akifanya mambo
yake na kuanzisha uhusiano na wanaume wengine maana yake amejitoa
mwenyewe kwenye mamlaka ya mumewe, hivyo hapo kunakuwa hakuna ndoa
tena,”alisema Shehe.