Baada ya msanii wa filamu Rose Ndauka kuthibitisha kuachana na aliyekuwa mchumba na mzazi mwenzake Malick aka Chiwa Man, Chiwa man pia ...
Akizungumza na 255 ya XXL, Chiwa Man amesema Ndauka ndiye aliyeamua kuondoka nyumbani walipokuwa wanaishi na kurudi kwao, lakini hakuwa tayari kusema chanzo.
“yeye mwenyewe ameamua kurudi kwao basi…” amesema member huyo wa kundi la zamani la muziki TNG.
Chiwa ameongeza kuwa kinachomuumiza hivi sasa ni kumkosa mtoto wake aliyempata na Rose.
“mtoto tu ndio kitu ambacho mi nataka, hicho tu ndio kitu ambacho mi sikipendi yaani ndo kitu ambacho kinaniumiza namuhitaji sana mtoto wangu, mi namwombea tu Mungu”.
Ndauka aliiambia Bongo 5 jana kuwa maamuzi ya kuachana yalifikiwa na wote wawili baada ya kukaa chini na kukubaliana japo hakuweka wazi sababu, na upande wa Malick pia hakuwa tayari kusema sababu.“Ni sisi tu wenyewe tumeamua tuwe hivyo lakini sina sababu zaidi…”.