Msanii wa Hip Hop, Rashid Makwiro 'Chid Benz' leo amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar...
Msanii wa Hip Hop, Rashid Makwiro 'Chid Benz' leo amepandishwa
kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na
kusomewa mashitaka matatu ya kukutwa na madawa ya kulevya, vifaa vya
kutayarishia, uvutaji wa madawa, usafirishaji na utumiaji wa madawa hayo
ambayo alikamatwa nayo kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Oktoba 23, 2014.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 11 mwaka huu na msanii huyo
ametupwa rumande kwa kukosa wadhamini.
Hata hivyo, atarudishwa kesho
kukamilisha taratibu za dhamana ambapo wadhamini wawili walitakiwa kutoa
Shs. Milioni moja kama bond.