PAMOJA na sheria za Ufaransa kuzuia watoto wa kambo kuoa mama zao wa kambo au watu wenye uhusiano wa kambo kuoana, mahaka...
PAMOJA na sheria za Ufaransa kuzuia watoto wa kambo kuoa mama zao wa
kambo au watu wenye uhusiano wa kambo kuoana, mahakama moja ya hapa
imefanikisha kuwapo kwa uhusiano wa ndoa kati ya mtoto wa kambo na mama
wa kambo.
Mtoto huyo Eric Holder, amemuoa mtalaka wa baba yake Elizabeth Lorentz mwenye umri wa miaka 48.
Imeelezwa kuwa mwendesha mashtaka wa eneo la Lorraine Ufaransa pamoja na kutokubaliana na uamuzi wa mahakama hiyo baada ya mabishano ya miezi kadhaa, haitaka rufaa.

![]() |
mtoto na mama yake wa kambo |
Watu hao wawili wamefunga ndoa kaskazini mashariki mwa kijiji cha Dabo, karibu na mji wa Metz.
katika hafla hiyo mtalaka wa mke huyo, baba yake mzaziEric, Mzee Holder alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa waliohudhuria shughuli hiyo..
Awali watu hao katika hekaheka za kisheria walifikisha suala lao hadi ofisi ya rais Francois Hollande, kuja kujibiwa kwamba sheria za Ufaransa haziruhusu watu wa kambo kuoana.