Mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Alex ambaye hivi karibuni Operesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ilimnasa akiwa kwenye danguro lililopo ...
Mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Alex ambaye hivi karibuni
Operesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ilimnasa akiwa kwenye danguro lililopo
Sinza Mapambano jijini Dar, anatarajiwa kupandishwa kizimbani kwa kosa
la kumjeruhi mmoja wa waandishi wa habari.
Alex akiomba msamaha ili aachiwe.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinadai kuwa, baada ya jamaa huyo
kunaswa kisha kuwafanyia vurugu waandishi waliokuwa wakitimiza majukumu
yao na kuwaharibia vitendea kazi vyao, polisi walifika eneo la tukio
kisha kumtia mbaroni.
...Akiwa chini ya ulinzi.
“Kesi ipo Kituo cha Polisi Mabatini, taratibu za kisheria zinaendelea
na wakati wowote atafikishwa mahakamani kwani ameniumiza sana na hali
yangu bado si nzuri, kwa hiyo ili iwe fundisho kwa wengine lazima
aadabishwe,” alisema mmoja wa waandishi hao.
Habari za mwanaume huyo kunaswa kwenye danguro ziliripotiwa jana kwenye gazeti ndugu na hili la Amani.
Habari za mwanaume huyo kunaswa kwenye danguro ziliripotiwa jana kwenye gazeti ndugu na hili la Amani.