UWEPO wa msanii Ali Kiba katika maziko ya aliyekuwa msanii wa TMK Wanaume Family, Ambikile Yesaya ‘YP’ ulisababisha waombolezaji weng...
UWEPO
 wa msanii Ali Kiba katika maziko ya aliyekuwa msanii wa TMK Wanaume 
Family, Ambikile Yesaya ‘YP’ ulisababisha waombolezaji wengi kusahau 
kilichowapeleka kwenye shughuli hiyo na kutumia muda mwingi wakijadili 
juu ya upinzani wa Ali Kiba na Diamond.
Maziko ya YP yalifanyika juzi kwenye Makaburi ya Chang’ombe, Temeke 
baada ya kuagwa kwenye Viwanja vya TCC, Chang’ombe, ambapo Ali Kiba 
hakuwepo wakati wa kumuaga TCC lakini alifika katika eneo la makaburini 
na kushiriki kumwaga mchanga kaburini.
Mara baada ya Kiba kutokea, ghafla mazungumzo yalibadilika na 
minong’ono ikaanza kuhusu hoja ya Kiba na Diamond kuwa nani mkali, huku 
tukio la Diamond kuzomewa kwenye Fiesta likizungumzwa na wengi.
Ubishi huo ulianza kuwa mkubwa muda ulivyosonga mbele, lakini uliisha
 baada ya Kiba kuondoka eneo la tukio muda mfupi baada ya shughuli ya 
maziko kumalizika.
