Rapper Young Killer Msodoki, amedai kuwa video ya wimbo wake ‘Umebadilika’ aliomshirikisha Banana Zorro itakuwa...
Rapper Young Killer Msodoki, amedai kuwa video ya wimbo wake
‘Umebadilika’ aliomshirikisha Banana Zorro itakuwa bora zaidi kuliko
video zote alizowahi kufanya.
Video hiyo iliyoongozwa na Hefemi Studios imefanyika katika visiwa vya Mbudya jijini Dar es Salaam.
Msodoki ameiambia Kikwetu Blog kuwa uzuri wa video hiyo utachangiwa
na mandhari aliyoyatumia ambayo yatapendezeshwa na muonekano wa bahari
na fukwe za Mbudya, watu watakaoonekana na picha ujuzi wa Hefemi
anayesifika kwa video zake zenye ubora wa hali ya juu.
Rapper huyo mshindi wa tuzo za KTMA 2014 kwenye kipengele cha msanii
bora, anayechipukia amesema video hiyo inatarajia kutoka wiki mbili
kuanzia sasa.