Kundi la Weusi linaloundwa na Joh Makini, G Nako, Nikki wa Pili, Bonta na Lord Eyez liko mbioni kuzitoa video tatu za nyimbo zao ndani ...
Kundi la Weusi linaloundwa na Joh Makini, G Nako, Nikki wa Pili,
Bonta na Lord Eyez liko mbioni kuzitoa video tatu za nyimbo zao ndani ya
wiki hizi mbili kuanzia leo.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, msemaji wa kundi hilo Nikki wa Pili
amesema kuwa wataanza kuachia video za ‘Sitaki Kazi’, I See Me ya Joh
Makini na mwisho ‘Mavijanaa’ ambayo ni ngoma mpya ya G Nako
aliomshirikisha Nikki.
“Tunakuja na video tatu ndani ya wiki mbili (kuanzia wiki hii).
Kuanzia wiki hii zitaanza kutoka na itatoka mojamoja. Nafikiri
zitapishana kwa wiki wiki lakini tunatoa video tatu.” G Nako ameiambia
tovuti ya Times Fm.
Ameeleza kuwa video zote tatu zimefanywa na muongozaji wa Kenya, Enos
Olik aliyeongoza video ya hit yao ‘Gere’ na zimefanywa katika maeneo
tofauti, Arusha na Nairobi.
“Sitaki Kazi imefanyika maeneo ya karibu na mtaani kwetu. Na
nimefanya Arusha kwa kuwa ni rahisi kumove kwa kuwa kule ndiko
tumezaliwa kwahiyo ni rahisi kupata vitu vingi watu wengi wakatusaidia
tofauti na tukifanya sehemu nyingine. Ndio maana Sitaki Kazi na
Mavijanaa tumefanyia mitaa tuliuyozaliwa mimi na G-Nako. Tumefanyia
Kaloleni, Mjini, River Camp…” Ameeleza G Nako.
Video ya I See Me imefanyika jijini Nairobi, Kenya.