KITUKO! Beautiful Onyinye, Wema Abraham Sepetu ametoa kioja cha aina yake kwa kuangua kilio baada ya kuambiwa kuwa mbwa wake aliyepotea...
KITUKO! Beautiful Onyinye, Wema Abraham Sepetu
ametoa kioja cha aina yake kwa kuangua kilio baada ya kuambiwa kuwa mbwa
wake aliyepotea amepatikana na alipokwenda kumfuata akaambulia patupu.
Mbwa wa staa wa filamu Bongo, Wema Abraham Sepetu aliyepotea.
Tukio hilo lililowaacha watu midomo wazi lilitokea juzikati maeneo ya
kishua, Masaki jijini Dar, ambapo staa huyo alionekana kukatishwa tamaa
kwani alipokuwa anatoka nyumbani aliamini kabisa anakwenda kukabidhiwa
mbwa wake aitwaye Vani aliyepotea miezi michache iliyopita.
“Nilipoambiwa amepatikana kwanza nilijenga picha kwamba hatimaye
furaha yangu imerejea, nilianza kuvuta picha ya kipindi cha nyuma
alipokuwepo nyumbani lakini nilipokwenda nikakuta ndivyo sivyo,” alisema
Wema na kuongeza:
“Uwiiii jamani Vani wangu ndio sitomuona tena naumia sana kuondokewa
na Vani nitamkumbuka daima, sijui amekufa au vipi!” alisikika Wema kiasi
cha watu waliokuwepo eneo hilo kumshangaa wakijiuliza ni mbwa tu
aliyemsababisha alie kilio mithili ya kuomboleza.
Wema ametangaza dau la shilingi milioni moja kwa mtu yeyote
atakayefanikisha kupatikana kwa mbwa wake huyo ambaye mwenyewe anasema
alikuwa faraja kubwa kwake pindi anapokuwa nyumbani.