Archive Pages Design$type=blogging

WATOTO WAMWOKOTA BABA YAO AKIWA AMECHINJWA

MFANYABIASHARA aliyefahamika kwa jina la Melasi Lutebula Ndabi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa  Kamati ya Ulinzi  na Usalama Mtaa wa ...

MFANYABIASHARA aliyefahamika kwa jina la Melasi Lutebula Ndabi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa  Kamati ya Ulinzi  na Usalama Mtaa wa Muhimbili 2, Kata ya Pemba, Wilaya ya Temeke jijini Dar, ameuawa kwa kuchinjwa na watu  wanaodaiwa kufika kwake kwa ajili ya kukodi shamba la kulima matikiti.
Mwili wa Melasi Lutebula Ndabi ukiwa umetupwa baada ya kuchinjwa.
Habari zinadai kuwa, marehemu mbali na kuwa mfanyabishara na kiongozi katika eneo hilo, pia alikuwa akijishughulisha kwa kilimo na ufugaji, kazi ambazo amekuwa akizifanya tangu afike  katika eneo  hilo mwaka 2005.
Akizungumza kwa uchungu na Uwazi, mke wa marehemu aitwaye Rehema Shaban (pichani),  alisema siku za nyuma kuna watu watatu walifika nyumbani hapo wakihitaji kukodi shamba kwa ajili ya kulima matikiti.
Watu hao ambao inadaiwa si wakazi wa eneo  hilo na wala hawajulikani walisema wanatokea Kijiji cha Lisu wilayani  Nzega, Mkoa wa  Tabora  walielekezwa  kwa  marehemu huyo.
Ilielezwa kuwa, kwa mara ya kwanza watu hao walifika  nyumbani kwa marehemu Septemba 5, mwaka huu baada ya mazungumzo ya kina, marehemu aliwaonesha eneo la ekari tatu.
Mke na watoto wa Lutebula Ndabi wakiwa na uzuni.
Mke huyo alisema hata yeye tukio hilo limemchanganya kwani aliamini wale vijana walikuwa ni watafutaji na ndiyo maana mumewe aliwapa shamba, kumbe walikuja kutafuta roho ya mume wake.
Alisema tangu watu hao wafike, siku tatu mbele ndipo walipogundua mumewe amechinjwa na vijana hao watatu hawajaonekana tena. Alisema siku ya tukio, mume wake aliondoka na vijana hao kwa madai wanakwenda kumtolea pesa kwenye mtandao wa simu ili wamlipe kwa ajili ya shamba hilo.
Kwa mujibu wa Rehema, watoto wake wawili (mmoja miaka 7, mwingine 4) ndiyo waliogundua mwili wa marehemu baba yao akiwa amechinjwa walipokwenda kuchunga ng’ombe.
Jeneza la marehemu, Lutebula Ndabi.
“Nikiwa bado najiuliza aliko mume wangu, mara mtoto wangu Ashura (mkubwa) akaja anakimbia huku ana wasiwasi, akasema, mama nimeona shati la baba, ndala na mguu wake. Ndipo tukaenda huko na watu lakini Ashura  alikataa kufika kwa awamu nyingine.
“Tulipofika tuliukuta mwili wa mume wangu. Niliona amekatwa kichwani na pembeni kulikuwa na panga. Baada ya hapo nilihisi mwili ukiishiwa nguvu, sikujua nini kilichoendelea,” alisema mwanamke huyo.
Mpaka sasa Jeshi la Polisi Wilaya ya Temeke linawashikilia  watu watatu,
wawili wakiwa ni wale waliowakaribisha wale vijana huku mmoja wao akiwa mwenyeji wa kijiji cha jirani, alikamatwa kutokana na maelezo ya bahasha iliyokutwa kando ya mwili wa marehemu ikisema ‘kumbuka yaliyotokea mwaka 2013’ ambapo baadhi ya watu walisema mtuhumiwa huyo aliwahi kutofautiana na marehemu.

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: WATOTO WAMWOKOTA BABA YAO AKIWA AMECHINJWA
WATOTO WAMWOKOTA BABA YAO AKIWA AMECHINJWA
http://api.ning.com:80/files/YkTQKvQouuourEANbQRqsUyOioPnTmr1ICLxB6nreL2cgGTimiD-n-trUsGCvILt4tJ2sazOpADsW42psFM3pXBfuclmSZ2k/VIFOO.jpg
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/09/watoto-wamwokota-baba-yao-akiwa.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/09/watoto-wamwokota-baba-yao-akiwa.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago