Wasanii wa filamu wakiwemo Johari, Monalisa, Irene Uwoya, Odama, Richie pamoja na Jacob Stephan aka JB jana katika viwanja vya Biafra Ki...
Wasanii wa filamu wakiwemo Johari, Monalisa, Irene Uwoya, Odama,
Richie pamoja na Jacob Stephan aka JB jana katika viwanja vya Biafra
Kinondani jijini Dar es Salaam, wameendesha kampeni ya kuosha magari ili
kuchangisha fedha itakayowasaidia waathirika wa ajali za barabarari
waliolazwa kwenye wodi ya hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Akizungumza na Bongo5 kwenye banda la Jaffary Carwash ambapo shughuli hiyo ilipokuwa ikifanyika, JB alisema kama wasanii wana wajibu wa kufanya shughuli za kijamii ili kuisaidia.
“Sisi kama wasanii tunaonyesha tunaweza kutumia nguvu zetu kuosha
magari ili kupata pesa za kuwasaidia watu ambao wameathirika kwa ajali
za gari. Kwahiyo hii ni sehemu ya wajibu wetu, tunawakaribisha watu waje
waoshe magari yao,” alisema JB
Picha Na:- Bongo5