Wasanii mbalimbali wa filamu wakiwemo Elizabeth Michael aka Lulu, Kajala Masanja, Irene Uwoya, Monalisa, Jacob ...
Wasanii mbalimbali wa filamu wakiwemo Elizabeth Michael aka
Lulu, Kajala Masanja, Irene Uwoya, Monalisa, Jacob Stephan na wengine
Jumamosi hii wataungana pamoja na uongozi wa hospitali ya Muhimbili
maeneo ya Kinondoni Biafra jijini Dar es Salaam kuosha magari ili
kuchangia fedha za kusaidia waathirika wa ajali.
Akizungumza na Bongo5 leo, aliyekuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Unity,
Steve Nyerere amesema wameamua kufanya hivyo ili kusaidia wodi ya
wagonjwa wa ajali katika hospitali ya Muhimbili.
“Kweli zoezi linaanza leo, kama ilivyo kazi ya msanii katika jamii,
leo pale Biafra tutaosha magari ya watu mbalimbali ili kuchangisha pesa
za kusaidia wodi ya wagonjwa wa ajali katika Muhimbili. Kwahiyo pia
tutakuwa na uongozi wa hospitali kusaidia zoezi ili liende vizuri. Zoezi
hili ni la leo na kesho na baada ya hapo tutatoka pamoja na uongozi wa
hospitali ili kwenda kukabidhi mzigo huo kwa wahusika,” amesema Steve.