Watayarishaji na waigizaji wote wa Series maarufu yenye mikasa ya kigaidi “Homeland”, wako Cape Town, Afrika kusini waki...
Watayarishaji na waigizaji wote wa Series maarufu yenye mikasa ya
kigaidi “Homeland”, wako Cape Town, Afrika kusini wakikamilisha msimu wa
nne wa series hiyo inayosubiriwa kwa hamu.
November mwaka huu, watakamilisha miezi sita wakiwa Cape Town ambapo watakuwa wamemaliza kushuti msimu huo.
Katika video iliyowekwa kwenye mtandao wa Variety , waandaaji hao
wameeleza kuwa wameweza kuibadili mitaa ya Cape Town na kuivisha taswira
ya Islamabad, Kabul na Washington DC ili filamu hiyo iwe imebeba sehemu
tatu zenye uhalisia.
Wakizungumzia kiasi cha pesa walichotumia hadi hivi sasa, waandaaji
hao wamesema zaidi ya $100,000 (Sawa na Tsh.167, 050, 000) zimetumika
kwa ajili ya magari peke yake. Sasa tengeneza picha ya majengo na vyote
vitakavyoonekana!
Angalia Video hapa, Behind The Scenes na maelezo yao: