Director mkongwe wa filamu nchini, Jully Tax aliyetengeneza nyoka aina ya anaconda kwenye filamu ya ‘Saradini’ amealikwa nchini Afrika ...
Director mkongwe wa filamu nchini, Jully Tax aliyetengeneza
nyoka aina ya anaconda kwenye filamu ya ‘Saradini’ amealikwa nchini
Afrika Kusini kutengeneza kitu kama hicho.
Jully ni miongoni mwa wasanii waliopokoa tuzo za kifamilia za H.Baba Jumamosi iliyopita
Akizungumza hivi karibuni, Jully Tax amesema kuwa ni watu
wachache kwenye filamu zilizofanyika barani Afrika walioweza kufanya
hivyo.
“Nataka niseme mbele ya waandishi wa habari kwamba kama nasema uongo
wajaribu kuangalia tu, hakuna mwaafrika yeyote amefanikiwa kutengeza
nyoka anayefanana na Anaconda ambayo nilihojiwa South Africa ‘Watanzania
mnaweza’ nikasema ‘tunaweza’, akasema ‘Afrika kitu hicho hakipo’. Sasa
mimi nimetengeneza nyoka kama Anaconda lakini nilibishiwa kabisa Afrika
hatuwezi kufanya kitu kama hicho, sisi hatuna mitambo, hatuna vifaa,
mimi nikawaambia ‘tayari nimefanya’ na wao wakaniambia ‘umewezaje au
wewe mchawi’. Sasa hivi ninaposema hivi mwezi wa kwanza ndio nimeitwa
kule natakiwa niende. Nitaiongelea nchi yangu ninakotoka na nitaongelea
tuliambiwa Afrika hatuwezi sasa nimeweza hiyo picha hipo tayari na watu
wengi sana wametoa comment zao kwamba Tanzania tumeweza kufika hatua
fulani,” alisema Jully Tax.
Kitazame kipache kifupi cha video kinachoonesha nyoka huyo kwenye filamu ya Jully Tax.
Pia muongozaji huyo alisema anasikitishwa na pale anapotengeneza
filamu nzuri ili ziifikishe Tanzania mbali lakini zinafungiwa kutokana
na madai kuwa zinatisha.
“Nilikuwa naumia ndugu zangu, watangazaji wakikaa kwenye media
wanasema, ‘sisi watanzania tutafika mbali lini? Kufanya kama wazungu,
kufanya kama Nigeria. Unakuta mzungu anamkata mtu kweli mkono, aamkata
utumbo kweli. Watanzania hatuwezi, mtangazaji anatangaza hivyo. Sasa
tumekuja kuweza picha zinafungiwa. Sasa sijui walikuwa wanaongea kitu
gani? Tumeweza kufanya na picha zimefungiwa! Sasa mnataka tufike mbali
au? Nina filamu tatu zimefungiwa. Nilitengeneza Zombi, nimeambiwa
inatisha sana, na tulikuwa tunaambiwa hatuwezi. Mimi napata uchungu
nalia kwanini hatuwezi? Na nimeenda nje nikaambiwa hatuwezi kutengeneza
Anaconda na nikatengezeza, sasa nahisi na hii itafungiwa sasa si
nitalala njaa? Nahisi hii itafungiwa.”