Meneja mkongwe na muewezeshaji wa Mkubwa na Wanae, Said Fella amefunguka kuhusu njia alizotumia kutafuta nafasi ya...
Meneja mkongwe na muewezeshaji wa Mkubwa na Wanae, Said Fella
amefunguka kuhusu njia alizotumia kutafuta nafasi ya biashara ya wasanii
wake akiwemo ‘Shaa’ kulipwa pale kazi zake zinapowekwa YouTube.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Fella amesema yeye na Babu Tale
waliumiza kichwa baada ya kuona wasanii wa Kenya wanaingiza pesa hata
kama hawajatoa wimbo mpya, bila kutegemea shows na ndipo walipoamua
kusafiri hadi Nairobi kuhakikisha wanafahamu nini hasa cha kufanya.
“Kweli tukaenda Kenya, tukaenda kukutana watu tukawauliza ‘jamani nyie mnaendaje mbona sisi tukiwapelekea wenzetu wanaotuuzia ringtone hapa Tanzania hatupati faida ile’. Lakini unakuta Jua Cali au Nyota Ndogo kafanya muziki zamani lakini anaendelea kula faida.” Amesema Said Fella.

“Yaani tumesafiria tobo na ndio maana tumelipata tobo. Hata juzi kati
Babu Tale na Diamond walivyoenda Nigeria kwenda kusaka tobo…na ndio
maana tunasema timu yetu Saka Tobo ili kwenda kuangalia wenzetu
wanafanya nini na tunakwenda wapi. Kwa hiyo huwezi kumfuata tu mtu
ukamwambia ebwana tobo hili…waje tuwaoneshe. Watanzania tunapendana.”
Said Fella ameiambia tovuti ya Times Fm.
Shaa ambaye kimuziki anasimamiwa na Said Fella hivi sasa analipwa kwa kazi anazoweka kwenye channel ya YouTube.
Video yake ‘Sugua Gaga’ imevunja rekodi ya video za bongo flava kwa
kuangaliwa zaidi YouTube, hadi leo imeangaliwa zaidi ya mara 4,656,000.