TID ameingia kwenye studio ya B Records za Dar es Salaam na rapper wa Afrika Kusini, Tumi Molekane. Wimbo waliorekodi unaitwa ‘Bongo’. ...
TID ameingia kwenye studio ya B Records za Dar es Salaam na
rapper wa Afrika Kusini, Tumi Molekane. Wimbo waliorekodi unaitwa
‘Bongo’.
TID amesema kuwa rapper huyo alikuwa na shauku kubwa ya kufanya naye kazi.
“Mimi na Tumi tumefanya kazi moja nzuri sana studio jana,” amesema
TID. “Tumetoka late sana kama saa kumi hivi. Tumerekodi wimbo mpya ambao
unaitwa Bongo. Tulikuwa tunawasiliana muda mrefu kupitia social
network, tukapata nafasi baada ya kuingia Dar es salaam ndo tukaamua
kufanya kazi. Project iko mwishoni kumalizika leo nafikiri tunamalizia
kurekodi hajarudi zake South Africa kesho. Mimi nafikiri video yake
tunatakiwa tufanyie South Africa muda si mrefu. Jamaa yupo serious
kabisa na hii kazi.”
Naye Tumi ameandika; In studio with the very shirtless T.I.D hehe. For real, this dude is crazy talented.”