Jamani tubaki njia kuu!!! demu mmoja nchini kenya ameripotiwa kutembea na wanaume zaidi ya 300 wakati anajua kabisa ni muathiri...
Jamani tubaki njia kuu!!! demu mmoja
nchini kenya ameripotiwa kutembea na wanaume zaidi ya 300 wakati anajua
kabisa ni muathirika wa ukimwi. Demu huyo aliamua kuchukua uamuzi huo
mgumu kama njia ya kulipiza kisasi kwa wanaume baada ya yeye kufanya
mapenzi yasiyo salama na mwanaume yaliyopelekea kuambukizwa ukimwi.Mwanafunzi
huyu kutoka Karabak University katika jiji la Nakuru aliamua kufunguka
kupitia facebook na kusema “nimesikia watu mkisambaza kashfa. Mimi nina
kashfa kubwa zaidi nataka kuisema.” gazeti la daily post nchini kenya
liliripoti.Mwanafunzi huyu
aliliambia gazeti la daily post la kenya kwamba ana miaka 19 tu kwasasa,
na alikua ni bikira mpaka siku alipoenda club usiku na watu wa miaka ya
juu hapo chuoni kwake. Alipoamka aligundua mmoja wa watu hao alifanya
nae mapenzi bila ya yeye kujua sababu alikua amelewa kupita kiasi.
