Juma Nature amedai kuwa hafikirii kwenda kushoot video zake nje ya nchi kama wasanii wengi wa Tanzania wanavyofanya. Nature amesema anaa...
Juma Nature amedai kuwa hafikirii kwenda kushoot video zake nje
ya nchi kama wasanii wengi wa Tanzania wanavyofanya. Nature amesema
anaamini kuwa hapa nchini kila kitu kinawezekana.
“Mie video zangu zote nitafanyia hapa hapa labda nikienda huko Ulaya
kufanya show ndo nitaweza kufanya video lakini eti natoka hapa sijui
naenda kufanya huko video siwezi,” amesema Nature. “Hapa Tanzania nina
uhakika kuna vijana wengi sana wamesomea mambo ya production nawapo
vizuri inabidi tuwatumie hawa vijana na bongo. Kuna malocation ya ukweli
inatakiwa sisi ndo tutangaze nchi yetu na tamaduni zetu kwa kufanya
video hapa nyumbani. Lakini sisi tukienda kufanya video huko nchi za
watu tutakuwa tunawatangazia wao nchi zao, kwahiyo lazima tuwe wazalendo
na nchi yetu.”
Katika hatua nyingine, Nature amesema ni ngumu kutoa album tena kwa
sasa kwakuwa teknolojia imeharibu mfumo uliokuwa ukiwezesha kuuzwa kwa
album na msanii akapata faida.
“Unajua sasa hivi pamekuwa na technology sana tofauti na zamani. Sasa
hivi hata ukisema unatoa album haitafanya vizuri kama zamani. Na hii
Tanzania yetu ndo kabisaa atanunua mmoja halafu ataweka kwenye mtandao
wengine wataanza kudownload utajikuta hujafaidika na chochote inabidi
serikali itusaidie hilo suala,” amesema.
Kuhusu mikakati ya kundi lake la TMK Halisi, Juma Nature amesema:
Tupo na tunafanya kazi muda si mrefu tutatoa kazi mpya zinakuja.
Tulikuwa tunarekodi mangoma ya ukweli, najua Bongo5 mtakuwa wa kwanza
kupata hiyo midundo. TMK Halisi ipo na watu wapo wanapiga mzigo wala
haijafa tena tupo vizuri sana.”