MAHABATi! Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ amedhihirisha kuwa yeye ...
MAHABATi!
Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ amedhihirisha kuwa yeye
ni mwanamke tayari wa kuwekwa ndani baada ya kusema anajitahidi kila
siku katika suala la mapishi ili asimlishe viporo mwandani wake, Nasibu
Abdul, ‘Diamond’.
Akipiga domo na paparazi wetu, Wema alisema kama mwanamke anajua
thamani ya mwanaume siku zote hata kama ‘baby’ wake atarudi usiku,
lazima aingie jikoni kupika na haweki chakula kwenye ‘hot pot’.
“Siku zote si kwamba najisifia ila kwa jikoni ndiyo mwenyewe sasa kwa
nini nipike chakula halafu niweke kwenye hot pot? Kwangu siruhusu
kabisa itokee,” alisema Wema.