Rangi mpya ya kucha Ni mara chache sana utakuta mwanaume huwa anagundua kwamba leo umeweka rangi tofauti ya kucha au umeweka nzuri...
Rangi mpya ya kucha
Ni
mara chache sana utakuta mwanaume huwa anagundua kwamba leo umeweka
rangi tofauti ya kucha au umeweka nzuri,kwa asilimia kubwa ya wanaume,ni
nadra sana kushtukia kuwa leo kuna kitu tofauti kwa mpenziye haswa
tukiongelea kuhusu rangi za kucha zako za miguu au za mikono,haijalishi
mpenzi wake ametumia muda gani kujaribu kutengeneza kucha zake ili
apendeze au ametumia pesa ngapi kutengeneza kucha,ila most men wont even
notice all of that,labda unaweza sema ni jinsi wanaume walivyoumbwa kwa
kile kutoweza kujua tofauti ya rangi vizuri.
Usipopaka make-up

Mara
nyingi kwa mwanamke asipopaka make up,especially ukikutana na mtu
ambaye huwa mnakonana mara kwa mara, anaweza kukuuliza ,ni nini
tatizo,au maswali yakizushi kama mbona leo unaonekana umepooza,vitu kama
hivyo,nadhani asilimia kubwa ya wanawake wameshawahi kuulizwa maswali
ya kizushi kama hayo siku ambayo wanatoka bila kupaka make-up,ukweli ni
kwamba asilimia chache sana ya wanaume wanauwezo wakugundua kuwa mpenzi
wake amepaka make up au la!.
Kutonyoa nywele za miguuni
Ni
kweli kuwa wanawake wengi hutumia muda wao mwingi kuhakikisha kuwa
wananyoa vinyweleo vya miguuni,ili kuongeza urembo zaidi na kufanya aina
zote za massage,ila kwa wanaume kugundua kuwa ,leo mpenziye hajanyoa
vinyweleo vya miguuni ni nadra sana kutokea,asilimia kubwa wanaweza
wasiwe na ufahamu hata kama huwa unanyoa hivyo vinyweleo.
Pochi mpya
Kwa
wanaume wengi kwao Pochi ni pochi tu,na kama hujagundua hili ni kuwa
pale tu unapobadili size ya pochi,labda leo umebeba pochi kubwa na kesho
umebeba ndogo, ndio utakuta ni rahisi kugundua,tena hiyo hutokea mara
chache sana,ila kwa upande wa pochi mpya,?si rahisi kabisa kuweza
kugundua.hata kama amekariri aina zako zote za pochi ulizonazo,labda tu
umdokeze kuwa kama kuna kitu tofauti leo,ila apart from that,ni bahati
sana umkute mwanaume anajua hilo,labda ujifanye umesahau price tag ndio
agundue.
Kuvaa Hereni mpya
Asilimia
kubwa ya wanaume kwa hili ni vigumu sana kugundua,najua wanawake wengi
hujitahidi kubadili hereni mbali mbali za aina tofauti ,ila hapa bila ya
kuuliza kama umependeza!, sidhani kama kuna mwanaume anayeweza
ku-notice changes,na kama yupo ni wachache sana,mara nyingi kutiokea
kama mwanamke ambae hana kabisa tabia ya kuvaa hereni,siku akiamua kuvaa
hapo kuna uwezekano wakugundua.