Rich Mavoko amesema haikuwa kazi rahisi kukubali kukaa karibu na yule mnyama cheetah anayeonekana kwenye video ya wimbo wake mpya ‘Pach...
Rich Mavoko amesema haikuwa kazi rahisi kukubali kukaa karibu na
yule mnyama cheetah anayeonekana kwenye video ya wimbo wake mpya ‘Pacha
Wangu’.
Mavoko ameiambia Bongo5 kuwa awali aligoma kabisa. “Haikuwa rahisi
aisee,” amesema Mavoko. “Nakumbuka wakati tumefika pale, hali
ilibadilika ghafla cause plan ilikuwa ni kwamba cheetah apigwe shot za
peke yake akiwa anatembea, lakini Adam akabadilisha script, akasema
‘Mavoko inabidi uimbe na cheetah’. Mwanzo niligoma kabisa, ila baada ya
kunishawishi yeye na yule mama wa kizungu anayemfuga, ambaye akanipa
mifano akaniambia ‘mbona akina Burner Boy na Dbanj walishoot naye bila
kuogopa you can do it too’ ndo nikajikaza kisabuni ikabidi nikubali. Ila
haikuwa rahisi kwasababu yule cheetah ni wa kweli na ana meno, ila
nashukuru Mungu tulipata shot nzuri.”
Chini ni video ya wimbo wa Burna Boy ‘Don Gordon’ ambamo cheetah huyo anaonekana pia.
Watanzania wengi wa nje na ndani ya nchi wamempongeza Rich Mavoko kwa video nzuri iliyoshootiwa jijini Cape Town, Afrika Kusini.