Promota wa muziki na filamu anayefanyia kazi nchini Uingereza, Hadija Seif maarufu kama Dida Fashion amesema wapenzi wa muziki nchini Ui...
Promota wa muziki na filamu anayefanyia kazi nchini Uingereza,
Hadija Seif maarufu kama Dida Fashion amesema wapenzi wa muziki nchini
Uingereza wanampenda zaidi Alikiba kuliko Diamond.
Dida alisema hayo kwenye mahojiano na Bongo5 hivi karibuni. “Sio sasa
hivi tu, tangu zamani to be honest kwa UK Alikiba yupo juu zaidi,”
alisema.
“Sijui kwanini lakini kwa watu wenyewe ukisema labda kati ya Alikiba
na Diamond hapo nani aletwe, honestly watu wa UK yaani Alikiba sijui
aliwafanya nini lakini Alikiba UK is the best,” aliongeza.