Muimbaji wa kike, Dayna, amesema kuwa amejifunza kutosema mambo ambayo bado hayajakamilika. Dayna ames...
Muimbaji wa kike, Dayna, amesema kuwa amejifunza kutosema mambo ambayo bado hayajakamilika.
Dayna amesema kuwa kuna mambo ambayo aliyaahidi lakini bado hayajafanyika kutokana na sababu mbalimbali.
“Nina vitu vingi ambavyo nafanya na nimefanya ambavyo vingi vipo nje
ya hapa. Pia nimeshaweka connection na watu wa nje na kuna watu
nimeshaanza kuweka nao mawasiliano,” amesema Dayna. “Sasa hivi
nilichojifunza ni kwamba sitasema mambo ambayo hayajatimia, nitasema
mambo ambayo yametimia. Kama mimi kuna mambo ambayo niliyaahidi lakini
hayajatimia kutokana na vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wangu. Kwahiyo
nimeona ni bora kusema kitu ambacho kipo tayari ili kuepuka
kuwayumbisha watu wako,” ameongeza.
Katika hatua nyingine msanii huyo wa ‘I do’ amesema wasanii wa kike
wanahitaji msaada kutoka kwa wadau muziki hapa nchini ili kuupeleka
mbali zaidi muziki wao.
“Kukubwa ninachoweza kusema sisi kama watanzania na ni watoto wa kike
na tumeamua kujitoa na kufanya kazi nzuri za muziki, tunahitaji support
zaidi. Maana yake sisi peke yetu kwa nguvu zetu hatuwezi kufikia
malengo yetu ila kuna watu ambao tunawajua wadau ambao wanaweza
wakatusupport zaidi na tukafikia malengo yetu. Sina wasiwasi na
mashabiki wangu kwa sababu najua ni watu ambao wamekuwa wakinisupport
toka nimeanza mpaka sasa na ninawashukuru zaidi.”