Rapper wa kampuni ya Weusi, G-Nako anatarajia kuachia ngoma mbili kwa mpigo Jumanne ijayo. Awali ya hapo rapper huyo aliwahi kusem...
Rapper wa kampuni ya Weusi, G-Nako anatarajia kuachia ngoma mbili kwa mpigo Jumanne ijayo.
Awali ya hapo rapper huyo aliwahi kusema kuwa yupo kwenye
njia panda kuamua wimbo wake mpya wa kuachia kwakuwa amerekodi nyimbo
nyingi na kali.
Kutokana na hali hiyo, rapper huyo wa Arusha alisema anafikiria
kutumia watu wengine wamsaidie kuamua wimbo gani anaofaa kuutoa. “Mimi
mwenyewe kama nimepagawa fulani, nafikiria kuwa na kamati kunisaidia
kuamua ngoma gani natoa maana mimi mwenyewe zinanichanganya,” alisema
G-Nako.
Rapper huyo alisema hadi sasa amerekodi nyimbo tano mpya na bado
anaendelea kurekodi katika studio mbalimbali. Aliwataja watayarishaji
aliofanya nao kazi kwenye nyimbo hizo kuwa ni pamoja na Chizan Brain,
Paul Beatz na Nahreel.