Stori: Gladness Mallya na Mayasa Mariwata ILE ndoa iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda ...
Baada ya zoezi hilo kumalizika, wawili hao
na wapambe wao walikwenda katika Kisiwa cha Bongoyo, Dar kwa ajili
kupiga picha za ukumbusho. Kisiwa hicho kipo Kilomita 2.5 kutoka Pwani
ya Jiji la Dar.
“Jamani sijui balaa gani hili? Yaani
tumetumbukia baharini tukienda Bongoyo, viatu vimezama, nguo tulizovaa
zimelowa, tukaletewa nyingine, simu yangu pia iliingia majini lakini
tunamshukuru Mungu tuliokolewa na kuendelea na safari,”alisema Lucy
alipoulizwa na gazeti hili.
Lucy alisema hajui ni nini, kwani
alishangaa sana baada ya kutoka Bongoyo wakiwa maeneo ya Kinondoni kuna
gari lililoonekana kuwafuatilia toka mbali, liliwafikia na kuligonga
gari lililokuwa katika msafara wake waliokuwa wakichukua matukio kwa
kamera ya video, wakashuka na kuanza kuwafanyia fujo kisha wakawapora
kamera hiyo na kuondoka kwa kasi eneo hilo.
Mbali na misukosuko yote waliyopata siku hiyo, lakini maharusi hao walifanikiwa kufika katika Ukumbi wa Makumbusho uliopo Posta Mpya, Dar ambapo sherehe ya kifahari ilifanyika na kuhudhuriwa na marafiki wa bi harusi na viongozi kutoka serikalini.
Mbali na yote, shughuli hiyo ilikuwa na
vituko mbalimbali ambavyo viliwakosha waalikwa, ikiwemo watu wa kareti
kutoa salamu zao za kikomandoo, mtu wa mazingaombwe ya nyoka, wanenguaji
kutoka Kampuni ya Bia ya Windhoek kutoa shoo ya nguvu na msanii mkongwe
Bongo, Ummy Wenceslaus ‘Dokii’ kutumbuiza.
Msanii huyo alipata zawadi kedekede kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki zake. Mama yake mzazi aliyekuwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Ilala, Marietta Minangi alimzawadia kiwanja kilichopo Bunju jijini Dar huku baba yake mdogo (jina halikupatikana) akimpa mbuzi na ng’ombe wawili wa maziwa.Kaka yake alimkabidhi shilingi milioni tisa taslimu ukumbini hapo na kamati ya sherehe ilimpa shilingi milioni tatu bila kumsahau Dokii ambaye alimzawadia matofali 500 na mifuko 10 ya simenti.
Kutokana na thamani kubwa aliyonayo mzazi wake kwa kumzaa na kumlea vyema, Lucy alimfanyia ‘sapraizi’ mama yake huyo kwa kumpa zawadi ya gari aina ya Toyota Prado ambalo alimkabidhi mahali hapo.
“Namshukuru sana mama yangu kwa malezi mazuri aliyonipa mpaka sasa nimeolewa, sioni cha kumlipa kwa thamani kubwa aliyonayo kwangu, ila nimeamua kumzawadia gari aina ya Prado, japo ana gari lakini nimemzawadia hili ikiwa kama upendo wangu kwake,”alisema Lucy ambaye siku si nyingi anataraji kuondoka nchini kwenda Denmark kwa mumewe.