Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto anatarajia kuachia wimbo mpya mwezi ujao. Wimbo huo umetengenezwa na producer Alan Mapi...
Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto anatarajia
kuachia wimbo mpya mwezi ujao. Wimbo huo umetengenezwa na producer Alan
Mapigo katika studio zake mwenye Mpoto.
Akizungumza leo, afisa habari wa Mpoto Theatre Gallery,
Dominic, alisema wimbo Ndovelwa ni wimbo wa asili kama kawaida yake
ambapo ndani ya wimbo huo amemshirikisha msanii mkubwa wa hapa nchini.
“Mpoto yupo kwenye tour ya masuala ya afya huko mikoani ila kikubwa
ambacho amewaandalia mashabiki wa muziki wake ni wimbo ‘Ndovelwa’ mwezi
wa kumi. Pia huu wimbo ameshirikishwa msanii mkubwa, mambo mengine mengi
wadau wasubiri watakuja kuona tu,” amesema Dominic.