MWIGIZAJI wa Bongo Movie, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amewataka viongozi kuwa wakali pindi wanapobaini kiongozi mmojawapo anachakachua ...
MWIGIZAJI wa Bongo Movie, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amewataka viongozi kuwa wakali pindi wanapobaini kiongozi mmojawapo anachakachua fedha basi wamuadhibu iwe fundisho kwa wengine.
Mwigizaji wa Bongo Movie, Mayasa Mrisho ‘Maya’.
Maya aliyasema hayo juzikati alipoulizwa na paparazi wetu kuwa wana
mikakati gani kama mmoja wa wanakamati ya uchaguzi wa Klabu ya Bongo
Movie ambapo alisema, wanasikia aibu kuona watu waliowapitisha wao,
wanachafuliwa na baadhi ya viongozi.“Wanatakiwa kuwaadhibu ili tusiwe tunachafuka mara kwa mara kama hivi karibuni tumesikia watu wanaachia ngazi kuepuka kuchafuka,” alisema Maya.
Hivi karibuni Katibu wa Klabu ya Bongo Movie, William Mtitu alijiuzulu nafasi yake akidai kuna uchakachuaji wa fedha uliofanywa na baadhi ya viongozi.