MAKAVU! Msanii aliyefunga pingu za maisha juzikati na mwanaume mwenye asili ya Denmark, Janus Stanley Landrock, Lucy Komba amesema kadr...
MAKAVU! Msanii aliyefunga pingu za maisha juzikati
na mwanaume mwenye asili ya Denmark, Janus Stanley Landrock, Lucy Komba
amesema kadri siku zinavyozidi kwenda anazidi kunogewa na mapenzi ya
mzungu wake na kuwaona Wabongo si lolote kutokana na kuwa waongo.
Akieleza la rohoni mbele ya paparazi wetu, Lucy alisema anatamani
angefahamiana mapema na mzungu huyo kuliko kuyumbishwa na mapenzi ya
Kibongo ambayo yamejaa ahadi nyingi za uongo, tofauti na watu wa asili
hiyo ambao wana msimamo mkubwa katika mapenzi.
“Nilipopataka siyo siri nimefika, kama ulaghai nishakumbana nao sana
katika mapenzi ya Kibongo ambayo yalinikinaisha mno, lakini sasa sina
mawazo kabisa katika haya mambo, wenzetu hawapendi kuchepuka hovyo
akikupenda, anakupenda kweli,” alisema Lucy.