Archive Pages Design$type=blogging

MADAWA YA KULEVYA YAMETUCHAFUA UINGEREZA - PADRI

PAROKO Msaidizi wa Kanisa Katoliki Kipawa, Ilala jijini Dar es Salaam, Joseph Mashaka amesema biashara ya madawa ya kulevya imechafua ...

PAROKO Msaidizi wa Kanisa Katoliki Kipawa, Ilala jijini Dar es Salaam, Joseph Mashaka amesema biashara ya madawa ya kulevya imechafua sura nzuri ya Tanzania iliyokuwa nayo nje ya nchi hususan Uingereza, baada ya vijana wengi kujihusisha nayo kwa kusafirisha na kutumia.
Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki Kipawa, Ilala jijini Dar es Salaam, Joseph Mashaka akiongoza ibada.
Kiongozi huyo alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa ibada maalum ya kumuombea marehemu  Leberatus Damian Matemu (55), aliyefariki dunia Agosti 31, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Alisema wakati akianza kujifunza kazi ya upadri katika mojawapo ya nchi za Ulaya, Tanzania ilikuwa nchi yenye heshima kutokana na usafi wa wananchi wake na viongozi, sifa ambayo hivi sasa imetoweka kabisa.
Waumini wakisikiliza mahubiri ya Padri.
“Maadili tuliyokuwa nayo tangu na baada ya kupata uhuru yametoweka, hivi sasa tumepoteza uadilifu kiasi kwamba hata hatuelewi tunafanya nini,waumini wenzangu lazima tutambue kuwa kuna Mungu, tujiandae kwa kila  namna, kwa matendo mema ili hata  siku za mwisho tuweze kupokelewa  katika uzima wa milele,” alisema padri huyo.Alisema siku moja akiwa nje, alipoonyesha hati yake ya kusafiria na kuonyesha kuwa ni Mtanzania, alimwagiwa sifa nyingi za kuisifu nchi yetu kitendo ambacho kilimpa faraja kubwa, tofauti na hali inayoendelea hivi sasa.
Baadhi ya madawa ya kulevya yaliyowahi kunaswa.
“Lakini leo hii nchi yetu inasemwa vibaya, kitu ambacho si kizuri hata kwa vijana imekuwa ni gumzo, ninawaomba tupendane na kushirikiana kwa uadilifu kama zamani, tumche Mungu kwani hakuna ajuaye siku wala saa,” alisema.
Katika ripoti ya mwaka huu, Tume ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya kulevya ilitoa takwimu ya Watanzania 403 waliokamatwa na kuhukumiwa wakijihusisha na biashara ya dawa za kulevya sehemu mbalimbali duniani na wengine wakisubiri kuhukumiwa.

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: MADAWA YA KULEVYA YAMETUCHAFUA UINGEREZA - PADRI
MADAWA YA KULEVYA YAMETUCHAFUA UINGEREZA - PADRI
http://api.ning.com:80/files/A1Qs8*3Ts4zOzmb8YZfjLH9Gv70W6N26I3*xhuYbCM8iS9QPssgWdHjaXeTscpSNEMaoLmXGO7z*wiWVGNVYYg-kmmnmho2p/DSC_0042.JPG
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/09/madawa-ya-kulevya-yametuchafua.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/09/madawa-ya-kulevya-yametuchafua.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago