Msanii wa filamu, Lungi Mwaulanga ametoa kali baada ya kusema kuwa, bila kuvaa nguo zinazoanika baadhi ya sehemu zake ‘muhimu’ hasikii ...
Msanii wa filamu, Lungi Mwaulanga ametoa kali baada ya kusema kuwa,
bila kuvaa nguo zinazoanika baadhi ya sehemu zake ‘muhimu’ hasikii raha.
Akipiga stori na gazeti hili, Lungi alisema kutokana na hali ya joto
ya Jiji la Dar, kuvaa nguo nyingi mwilini ni sawa na kujipa karaha hivyo
hulazimika kuvaa vivazi vya kisasa zaidi.
”Najua kuna ambao wanakereka na uvaaji wangu lakini nadhani hawana
sababu ya kukereka. Napenda kuvaa ninavyojisikia kwa hiyo hata
nikivaaje, ni mimi na maisha yangu,” alisema Lungi.
ODAMA: NAANZAANZAJE KUMFICHA BWANA’NGU?
ODAMA: NAANZAANZAJE KUMFICHA BWANA’NGU?
Stori: Rhoda joSIAH
Mwanadada anayeuza nyago kwenye filamu za Kibongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amekanusha tuhuma ya kumficha mwandani wake na kufunguka kuwa, marafiki na familia yake wanamjua hivyo haoni sababu ya kumfanya kila mtu amjue.
Mwanadada anayeuza nyago kwenye filamu za Kibongo, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amekanusha tuhuma ya kumficha mwandani wake na kufunguka kuwa, marafiki na familia yake wanamjua hivyo haoni sababu ya kumfanya kila mtu amjue.
Odama alikuwa akizungumzia madai ya kumficha mwanaume aliyezaa naye
huku baadhi wakisema, hataki mtu yeyote amjue kwani ni mume wa mtu.
“Hivi naanzaanzaje kumficha mwandani wangu? Halafu nimfiche ili
iweje? Ndugu na marafiki zangu wanamjua, wasiomjua wawe na subira, kila
jambo lina wakati wake,” alisema Odama ambaye juzikati alinaswa akiwa
‘very close’ ukumbini na mwanaume aliyefahamika kwa jina la Daudi ambaye
ni mume wa mtu.