Star wa filamu nchini aliyejaaliwa mvuto wa kipekee, Lulu Elizabeth Michael anadaiwa kutodumu na mwanaume sababu y...
Star
wa filamu nchini aliyejaaliwa mvuto wa kipekee, Lulu Elizabeth Michael
anadaiwa kutodumu na mwanaume sababu ya kuendekeza ubabe na kutaka
kum-control
mwanaume anayekuwa naye.
Inadaiwa Lulu hataki mchezo, mwanaume akishakuwa nae basi lazima ahakikishe hafurukuti. Taarifa zinadai kuwa
miezi ya hivi karibuni alikuwa na jamaa mmoja mdogo kimapenzi akammwaga
na baada ya muda akawa anatoka na tajiri mmoja wa madin toka
Arusha lakini tajiri huyo alinyoosha mikono juu baada ya Lulu kama
kawaida kuruhusu majeshi yake yam-control jamaa huyo.
Chanzo kimoja
kikizungumza kwa sharti la kutotajwa jina kimesema:
" Lulu ni mtu mwenye kisirani kwa wanaume, hadumu nao, wengie wanaokuwau nae
ni wale wavumilivu sana. Nadhani ana matatizo ambayo yanahitaji mtaalam
wa saikolijia ya mahusiano, akizinguliwa tu hachelewi kuvunja simu na
kurejesha kila kitu alichokuwa amepewa"