Archive Pages Design$type=blogging

KAJALA, HIVI HUKUJIFUNZA KITU KWA WEMA?

KAMA mwandishi, sijawahi kukutana na Kajala Masanja na kufanya mazungumzo naye, lakini kama mdau nimeona kazi kadhaa za muigizaji ...



KAMA mwandishi, sijawahi kukutana na Kajala Masanja na kufanya mazungumzo naye, lakini kama mdau nimeona kazi kadhaa za muigizaji huyu mwenye jina kubwa katika Bongo Movie.Anajitahidi kuigiza na katika uhalisia wake, huyu ni miongoni mwa wadada wanaoweza kuibeba tasnia hii na kuifikisha katika levo zingine za mbali na kuiletea sifa nchi yetu.

Nimewahi kusoma simulizi juu ya maisha yake, inasisimua sana, hasa alipokuwa akizungumzia sakata lililosababisha yeye na mumewe kukamatwa, kufikishwa mahakamani na hatimaye kuhukumiwa jela. Amepitia maisha yanayotosha kumpa mifano na mafunzo mengi ya maisha.
Kama siyo shoga yake Wema Sepetu kumlipia fedha za faini alipohukumiwa pale Kisutu mwaka mmoja uliopita, hivi sasa tungekuwa angalau tumeanza kumsahau Kajala, kama ilivyo kwa mume wake Agostino Faraji.

Lakini unapomuona maisha anayoishi hivi sasa, unashindwa kujizuia kujiuliza kama ana chochote cha kujifunza na kujutia katika maisha anayopitia, hasa katika matumizi ya fedha.Wanaomfahamu vizuri wanasema hivi sasa msichana huyu ana fedha za kutosha, kiasi cha kumfanya atembee akiwa na wapambe, si unajua tena kibongobongo?
Sijajua ni fedha kiasi gani, lakini unapomuona msichana kama Kajala, anakwenda kumtunza mtu burungutu la shilingi laki sita na ushee, ni lazima ukubali kuwa anazo za kutosha.

Enzi za ujana wetu, tulizoea kuwaona watu walioitwa Mapedeshee wakifanya madoido hayo katika kumbi za starehe na kwenye mikusanyiko. Na ninawakumbuka bado, akina Fikiri Madinda, Juma Banatoz ‘JB’, Papaa Msofe, Muzamil Katunzi, Papaa Chosta, Hussein Makabyureta, Rama Mutoto ya Ng’ombe, Jack Pemba ‘JP’ na wengineo wengi wa enzi zao.
Sitaki sana kuingia kwa undani kujua nini kimewasibu watu hawa kwa sasa, lakini ushahidi wa mazingira unaonyesha jamaa wamebadili staili ya maisha, bila shaka baada ya kugundua walikuwa wanapotea, kwa sababu walikuwa wanayanunua majina yao kwa bei kubwa sana.

Shoga yake Kajala, Wema Sepetu, miezi michache iliyopita naye alikuwa katika hali kama hiyo, akitapanya fedha kwa staili ya kutembea na wapambe wengi, huku akigharamia matumizi yao, hata yale yasiyo na msingi.
Simfundishi namna ya kutumia fedha zake, lakini ni ushauri tu ambao anaweza kuufuata au kuushiti. Pesa haitoshi. Anaweza kuziona nyingi leo, lakini sidhani kama zinaweza kufika kesho.
 
Katika kutengeneza maisha, kesho iko mbali sana, lakini kwenye matumizi, kesho ni kufumba na kufumbua tu.
Watu wenye fedha zao tunaowajua, hawana ujuha wa kumwaga hela ovyo kwa lengo la kujitangaza, badala yake kama kurudisha sehemu ya hela kwa jamii, hula na watoto yatima, wazee wasiojiweza na wakati mwingine kuwapa mahitaji muhimu kama vyakula na mavazi.

Kajala bado ni binti mdogo. Kuwa na shilingi milioni 50, 100 au bilioni moja siyo kufika, bali ni mwanzo mzuri wa kutengeneza maisha ya baadaye. Nimshauri awekeze katika kilimo, majengo au ufugaji, uwekezaji ambao baada ya miaka michache, fedha zitaanza kutiririka bila kikomo na hivyo kumpa uhakika angalau.

Hana sababu ya kujenga jina kwa sababu tayari analo ila ana ulazima wa kujenga maisha kwa vile hana. Sifa za kijinga ndiyo zinazowasumbua sana wasanii, wanashindwa kuyajenga maisha yao kwa pesa wanazozipata kutokana na fursa mbalimbali wanazokutana nazo.

Hela zinapokuja hazipigi hodi na uzuri wake zinapoondoka, mwenye kuzimiliki anajua kuwa zinaondoka. Kajala anamjua Bill Gates? Ni tajiri wa kutupwa, lakini kila siku anakuwa mtu wa kwanza kufika ofisini kwake, kuhakikisha utajiri wake hauyumbi.
Leo mdogo wangu Kajala umepata mkondo unautumia kutafuta sifa, badala ya kujijengea misingi imara ya maisha yako ya baadaye!

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: KAJALA, HIVI HUKUJIFUNZA KITU KWA WEMA?
KAJALA, HIVI HUKUJIFUNZA KITU KWA WEMA?
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjKb57iyqRsDkNfMFBOyGixGimcQzJ-V_FsNc5twPFAUf554aM4cj3PvTvISsVZ4iElWVRMgCEO1g-HxPNCBlaXAwO9EKzVt8K3wd2kFJRXmsgZ6zz6dCTyRfdkFIoY7jvD95EWdZTN3iQ/s640/KAJALA2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjKb57iyqRsDkNfMFBOyGixGimcQzJ-V_FsNc5twPFAUf554aM4cj3PvTvISsVZ4iElWVRMgCEO1g-HxPNCBlaXAwO9EKzVt8K3wd2kFJRXmsgZ6zz6dCTyRfdkFIoY7jvD95EWdZTN3iQ/s72-c/KAJALA2.jpg
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/09/kajala-hivi-hukujifunza-kitu-kwa-wema.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/09/kajala-hivi-hukujifunza-kitu-kwa-wema.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago