Wasanii wengi wa bongo siku hizi hawawaandikii bure nyimbo wasanii wenzao sababu imegeuka kuwa biashara inayoli...
Wasanii wengi wa bongo siku hizi hawawaandikii bure nyimbo
wasanii wenzao sababu imegeuka kuwa biashara inayolipa, kitu ambacho
kimemkuta Jux pia ambaye single yake mpya ‘Sisikii’ iliyotoka jana
ameandikiwa na rapper Mabeste.
Akizungumza wakati anautambulisha wimbo huo jana kupitia XXL ya
Clouds Fm, Jux amesema alipomfata Mabeste na kumwomba amwandikie wimbo
alimwambia atafanya hivyo lakini anataka alipwe kwa kazi hiyo.
“Tukaongea na mabeste akasema gharama zake, akasema mi nitaandika
lakini siandiki ngoma bure Jux, nikasema aah huu si muziki bwana,
muziki unajua uki invest na kama kitu kizuri hujui baadae itakuwa vipi,
nikamwambia sawa akaniambia price yake anayofanya ye Mabeste kuandika
nyimbo nikamwambia fresh akachora ngoma na kweli kabisa nikaimba
ikaisha…studio tulikuwa mimi Bob na Manecky”.
Jux amesema kuwa amemlipa Mabeste shilingi milioni mbili (2,000,000/=) kwaajili ya kuandikiwa wimbo huo.
“2 million, serious Mabeste aliniambia hivyo sababu ana nyimbo nyingi sana, na kuna nyimbo nyingine mimi nilishindwa kuzichukua kutokana na bajeti yangu…nikampa hela akachora baadae tukatoka nikaenda kwenye ATM nikamtolea hela nikammalizia hela yake”.
“2 million, serious Mabeste aliniambia hivyo sababu ana nyimbo nyingi sana, na kuna nyimbo nyingine mimi nilishindwa kuzichukua kutokana na bajeti yangu…nikampa hela akachora baadae tukatoka nikaenda kwenye ATM nikamtolea hela nikammalizia hela yake”.
Aliendelea,
“Mimi sikutegemea kama angeniambia hiyo hela hata mimi mwenyewe
nilishangaa , nime bargain hadi kufika hapo ana nyimbo nyingine ambazo
mimi nilikuwa nazitaka kabisa nyimbo kali sana Mabeste anafika hadi 4
million, lakini nyimbo yangu akasema kwa hii nyimbo yako kwasababu beat
ni yako, melody umetoa hiyo hapo kama hutaki basi, afu mi nikaangalia
nikasema sasa kama mtu unaweza ukalipa video hela nyingi…kwahiyo mi
nikaona nataka kitu kipya, muziki mpya ambao kila siku sio yule yule Jux
nikamwambia sawa Mabeste.”
Baada ya wimbo kukamilika Jux aliridhika kupata kile alichokilipia, “kwa sababu nyimbo nilivyoiskia wakati imeisha nikaona yah this is a song I needkwahiyo sawa Mabeste umefanya kitu”.
Baada ya kulipishwa na Mabeste, Jux pia amemwimbia Mabeste chorus ya wimbo wake mpya ambao naye amemlipisha.
“Kuna chorus yake ambayo inakuja mi nimemfanyia Mabeste..hiyo ni
biashara yeye ameni charge na mimi nimemcharge tunafanya kibisahara
zaidi”.