MISS Progress International, Julieth William ambaye ni Mkurugenzi wa Progressive Fo...
MISS Progress International, Julieth William ambaye
ni Mkurugenzi wa Progressive Foundation amesema kamwe hawezi kuwasahau
walemavu wa ngozi kutokana na mateso wanayopata ya kukatwa viungo na
kuuawa ambapo kila wakati huwa anawapatia msaada.
Miss Progress International, Julieth William akiwabeba watoto wawili wenye ulemavu wa ngozi.
Akizungumza hivi karibuni baada ya kutoa msaada wa vifaa mbalimbali
vya shule katika kituo cha walemavu wa ngozi Magomeni, Dar Julieth
alisema katika maisha yake ameshajiapiza kwamba kila atakachopata lazima
agawane na wenzake ambao ndiyo hao walemavu wa ngozi.
“Ninajitolea kwa kila ninachoweza na ninachokipata ninagawana na wenzangu kwani hawa ni binadamu kama sisi na ninaumizwa sana na watu wanaowatesa kwa kuwakata viungo na kuwaua kwani nao wanastahili kuishi kwa uhuru kama sisi,” alisema Julieth.
- GPL